Zahera amtema Mmoja Yanga, Huyu naye anusurika

Zahera amtema Mmoja Yanga, Huyu naye anusurika

0

Zahera amtema Mmoja Yanga, Huyu naye anusurika

Unaambiwa Kocha Mpya wa Yanga hataki tena Masihara na anataka kukijenga Vyema Kikosi chake ili aweze kufanya vizuri msimu ujao wa Kigi kuu soka ya Tanzania bara na Michuano Mingine ambayo Yanga Itashiriki.

> Magazeti ya michezo leo <

Mwinyi Zahera ambaye juzi alisaini mkataba wa Miaka 2 kuifundisha Yanga taarifa zinadai aliomba Mikataba ya wachezaji wote na Alipofikia kwenye mkataba wa Donald Ngoma alitaka ufafanuzi juu ya Mchezaji huyo.

Zahera akaambiwa amecheza mechi chache tu za mwanzoni mwa Msimu na toka hapo amekuwa majeruhi mpaka leo, Zahera aliwauliza viongozi wa Yanga kama kuna uwezekano wa Ngoma Kupona akaambiwa bado haieleweki.

>Manara : Rais kanisisitiza jambo hili mara 3 <

Baada ya kusikia haieleweki Zahera aliwaomba viongozi kukaa na Ngoma na kuvunja naye mkataba kwani hana faida kwa Yanga kwasasa.

TAMBWE NAYE ALIKUWA APIGWE CHINI

Katika hatua nyingine  msomaji wa Kwataunit Mshambuliaji raia wa Burundi Amis Tambwe naye alionekana kuwa ni moja ya wachezaji waliocheza mechi chache huku sababu ikiwa ni majeruhi.

Lakini kocha aliamua kumpa muda wa kumuangalia Tabwe kutokana na Kurejea kwake Kikosini na Kuanza kupata nafasi ya Kucheza.

Yanga kwasasa inahaha kuhakikisha inaboresha kikosi chake kutokana na kutofanya vizuri kwenye Ligi msimu huu na Kuwaacha watani wao Simba wakifanya vizuri kiasi cha kuwapokonya Ubingwa wao.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY