Simba yaifananisha Kagera Sugar na Somalia

Simba yaifananisha Kagera Sugar na Somalia

0

Simba yaifananisha Kagera Sugar na Somalia

Klabu ya Simba Kupitia kwa Afisa habari wake Haji Manara wameifananisha klabu ya Kagera sawa na Somalia ambayo imewahi kutangaza Vita na Nchi kama Marekani.

Haji Manara msomaji wa Kwataunit amefunguka kuwa Wanasikia tambo za Kagera kutibua sherehe za  Ubingwa wao Kwa kuwafunga Jumamosi lakini hawana Hofu juu ya Hilo kwani sio kazi rahisi kwa Kagera Sugar  kuwafunga kwani hata Somalia wamewahi kutangaza Vita kwa Taifa lililovizuri kijeshi kama Marekani.

Simba itacheza na Kagera Sugar Jumamosi 19 May 2018 hii katika uwanja wa Taifa kuanzia Majira ya saa nane mchana huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY