Neema yazidi kumwagwa Simba Sc

Neema yazidi kumwagwa Simba Sc

0

Neema yazidi kumwagwa Simba Sc

Mara baada ya Simba kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu msimu wa 2017/2018 huku ikitwaa Ubingwa na mpaka sasa ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja imeelezwa neema imezidi kumwagwa ndani ya Simba.

Kwamujibu wa Gazeti la Dimba la Jumatano tajiri wa Simba Bilionea Mohammed Dewji maarufu zaidi kama Mo ndiye amezidi kuleta neema zaidi kwa Kikosi cha Wachezaji wa Simba.

Taarifa hiyo inadai Mo Amewataka viongozi kutogusa fedha ya Ubingwa Takribani Shilingi Milioni 80 za Kitanzania na badala yake fedha yote wapewe wachezaji wa Simba kwani ndiyo waliovuja jasho kupigania Ubingwa Huo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY