Matokeo Yanga vs Rayon Sports 16 May 2018

Matokeo Yanga vs Rayon Sports 16 May 2018

0

Matokeo Yanga vs Rayon Sports 16 May 2018

Matokeo Yanga vs Rayon Sports kutoka Rwanda 16 May 2018 moja kwa Moja kutoka Uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam, Karibu Uungane na Kwataunit.com

> Habari za Michezo <

Timu tayari ziko uwanjani tayari kwa Pambano

Mechi imeanza katika uwanja wa Taifa

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Sekunde ya 30 Hassan Kessy anaingia kwa Kasi na Kusababisha Kona

Inapigwa Kona ambayo inakosa madhara.

Dakika ya 2

Yanga 0 – 0 Rayon

Dakika 5 bado ni 0 kwa 0

Yanga wanaonekana kucheza kwa Kasi sana katika dakika za Mwanzo

Dakika 10

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Dakika ya 14 Alijaribu kupiga Penetration Pass lakini mabeki wa Rayon wanazuia

Dakika 15

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Dakika 20 bado matokeo ni duara kwa duara

Dakika ya 23 Hassan Kessy ambaye leo anacheza vizuri anaonekana kumlaumu mwamuzi kwa Kutoona Faulo aliyochezewa, bado ni 0 kwa 0

Dakika ya 25 Juma Mahadhi anajaribu shuti golini kipa anauona Mpira na Kuudaka

Dakika ya 27 Rayon wanaweka Mpira Nyavuni Line Two anasema mpira Ulikuwa umetoka kabla, Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Dakika ya 29 Hassan Kessy anapanda na Mpira anapiga shuti mpira unapaa Juu

Dakika 35

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Yanga wanasogea mpaka kwenye Boksi lakini wanashindwa Kumalizia shughuli

Dakika ya 38 Free Kick kuelekea lango la Rayon Sports, Unapigwa Mpira na mwashiuya Mita 22 lakini Kipa wa Rayon anakuwa kwenye position nzuri ya Kuudaka

Dakika ya 39 Kelvin Yondani anatoa Mpira Uliokuwa ukielekea lango la Yanga na Kuwa Kona

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Dakika ya 42 Anaingia kwa kasi Juma Mahadhi anapiga Krosi lakini Kipa wa Rayon Erick anaidaka

HALF TIME

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha Pili kinaendelea

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Dakika ya 48 Yanga wanafanya shambulizi zuri ambalo Geofrey Mwashiuya almanusra aipatie Yanga bao, Beki anaokoa kabla ya mpira kuvuka mstari wa goli

Dakika ya 52 Rayon wanawakosa Yanga bao.

Dakika 55

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Dakika ya 58 Hassan Kessy anapewa kadi ya njano baada ya kucheza rafu mbaya

Dakika ya 60

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Dakika ya 64 Rayon wanapata nafasi nzuri ya Kufunga Diara anashindwa kutoa pasi nzuri ya Mwisho kwa mwenzake

Dakika ya 66 Thaban Kamusoko anatoka anaingia Raphael Daud Washabiki wanaonekana kutopenda Hii Sub, Kamusoko amecheza katika kiwango bora sana leo

Dakika ya 68 Obrey Chirwa anachop mpira Unagonga mwamba wa Juu ilikuwa nafasi iliyotengenezwa na Raphael Daud aliyepiga mpira kwa Mahadhi, Mahadhi akamtengea Chirwa

Dakika 75

Yanga wanakoswa goli ambalo ni umakini tu wa Straika wa Rayon umewaangushwa Rayon.

Dakika ya 78 Youthe Rostand anafanya kazi ya ziada kuokoa shambulizi la Rayon

Dakika ya 79 Raphael Daud anapewa kadi ya Njano kwa Mchezo usio wa Kiungwana, Ni Free kick kuelekea Yanga

Yanga 0 – 0 Rayon

Dakika ya 83 Obrey Chirwa anatoka anaingia Amis Tambwe

Dakika ya 88 Geofrey Mwashiuya anatoka anaingia Emmanuel martin

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

Yanga wanapata Kona ya Dakika za Mwisho, inapigwa Kona Inakosa Madhara

FULL TIME

Yanga 0 – 0 Rayon Sports

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY