Maoni ya Edo Kumwembe kiwango cha Yanga na Kuhusu Nsajigwa

Maoni ya Edo Kumwembe kiwango cha Yanga na Kuhusu Nsajigwa

0

Maoni ya Edo Kumwembe kiwango cha Yanga na Kuhusu Nsajigwa

Mchambuzi maarufu wa Soka nchini Edo Kumwembe amesema Washabiki ambao wamekuwa wakilaumu juu ya Uwezo wa waalimu wa Yanga hasa Shadrack Nsajigwa ni kama wanamuonea Tu kwani kikosi cha Yanga cha sasa ni wazi hakiko vizuri.

Edo amesema kikosi cha Yanga cha sasa huwezi ukakilinganisha na Kile cha Yanga cha miezi 32 iliyopita kilichokaribia kumtoa Al Ahly ya Misri mjini Cairo.

Edo ambaye amekuwa muwazi sana anapochambua soka ameendelea mbele na Kusema licha ya kikosi cha Yanga kuwa dhaifu kikosi hiko kimezidi kuwa ovyo kutokana na Mdororo wa Uchumi uliopo ndani ya Klabu.

Baada ya Mchezo kati ya Yanga na Rayon Sports msomaji wa Kwataunit baadhi ya washabiki wa Yanga walionekana kumnyooshea Kidole Shadrack Nsajigwa kwa Kutokuwa na Imani na Uwezo wake wa Kuifundisha Yanga.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY