Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Rayon Sports 16 May 2018

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Rayon Sports 16 May 2018

0

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Rayon Sports 16 May 2018

Yanga leo 16 May 2018 Inashuka dimbani kucheza mechi yake ya Pili hatua ya Makundi dhidi ya Rayon Sports katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo hiki ni Kikosi cha Utabiri kinachoweza kuanza

Golini : Youthe Rostand amekuwa kipa namba moja kwenye kikosi cha Yanga michuano ya ndani na hata ya kimataifa bila shaka na leo ataiongoza Yanga

> Habari za Michezo <

mabeki wa pembeni : Namba 2 Hassan Kessy bila shaka atapewa nafasi ya kuanza katika mchezo wa leo huku shavu la Kushoto Gadiel Michael Kamagi.

Mabeki wa Kati : Kuna walinzi wanne wanaoweza kucheza nafasi Hii Yondani,Cannavaro,Ninja na Dante lakini kwa mechi ya leo kama wako fiti basi Kelvin Yondani na Andrew Vicent wananafasi Nzuri zaidi ya Kuanza.

Viungo wa Kati : Namba 6 papy Kabamba Tshishimbi ananafasi nzuri zaidi ya Kuanza katika Kikosi cha yanga cha leo akisaidiana na Kati ya Pius Buswita au Thaban Kamusoko.

Mawinga : Kuna namba ambayo ni kama ishapata mtu wake  hii ni winga ya kulia ambayo winga Yusuph Mhilu amekuwa akiitendea haki, Kasi yake na uwezo wa Kufanya maamuzi ya haraka inamsaidia sana kuendelea kuaminiwa

Huku winga ya Kushoto kukiwa kuna option kama 3 Hivi either Ibrahim Ajibu ambaye amekuwa akianzia Kushoto mechi kadhaa zilizopita au wenye asili ya Namba hiyo Emmanuel Martin au Geofrey Mwashiuya.

Lakini Ibrahim Ajibu ananafasi zaidi ya Kuanza kama atakuwa yupo Fiti kwani Emmanuel na Mwashiuya ni wazuri wanapotokea benci kutokana na kasi wanayokuwa nayo wanapoingia.

Washambuliaji : Hapa nafasi hii msomaji wa Kwataunit.com ni ya Obrey Chirwa kama namba 9 na namba 10 Amekuwa akicheza Raphael Daud ambaye ameonekana kuwa na kasi zaidi anapocheza eneo la Mbele.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY