Matokeo Welayta/Wolaita Dicha vs Yanga 18 April 2018

Matokeo Welayta/Wolaita Dicha vs Yanga 18 April 2018

0

Matokeo Welayta/Wolaita Dicha vs Yanga 18 April 2018

Matokeo Kati ya Welayta Dicha iliyonyumbani kuwakaribisha Yanga kutoka Dar Es Salaam Tanzania uwanja wa Kimataifa wa Hawassa Mjini Hawassa Ethiopia.

Soma habari za yanga >> Hapa <<

Timu zinaingia uwanjani tayaro kwa Pambano mjini Hawassa Ethiopia

Tayari mechi Imeanza Kati ya Welayta Dicha na Yanga

Welayta Dicha 0 – 0 Yanga

Dakika ya 2 Welayta Dicha wanapata bao kupitia Mpira wa kona kimo cha Mbuzi.

Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 4 Yanga wanajaribu Kutulia na Kupiga Pasi za hapa na Pale

Dakika ya 9 Yanga wanapata Mpira wa Kurusha karibu na goli la Dicha  lakini unakosa madhara

Bado Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 12 Dicha wanapata Kona Nyingine lakini Inatua Mikononi mwa Youthe Rostand Jehu

Jaco Araphat wa Dicha anaonekana kuwa Msumbufu sana kwa Yanga mpaka sasa

Dakika 15

Welayta Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 16 Yusuph Mhilu alijaribu Kuingia kwa Kasi beki akaokoa Mshambuliaji wa Yanga akpiga shuti mpira Ukapaa Juu

Dakika ya 20

Welayta Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 22 Wolaita Dicha wanazipiga zile zao kampa kampa tena hali inayoamsha shangwe kwa washabiki wao wengi waliojaa uwanjani kuwashangilia

Dakika ya 23  wachezaji wengi wa Yanga wamerudi Nyuma wakimuacha Chirwa peke yake Mbele

Dakika ya 25 Obrey Chirwa katikati ya mabeki wa Dicha anapiga Shuti linaenda NJE ya Lango

Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 26 Chirwa anakipimbia na Kupiga Krosi ambayo bado kidogo Dicha wajifunge mpira unakuwa ni kona, Kona Inazaa faulo aliyochezewa Shaibu Ninja.

Dakika ya 28 Inapigwa Faulo na Mwinyi Haji lakini inakosa madhara kwa Dicha

Dakika 29 Yanga wanakoswa Goli la Wazi baada ya Walinzi kuzubaa kuondoa Mpira wa hatari uliokuwa unazagaa langoni mwao

Dakika ya 32 Yanga wanapata Kona inakosa kuwa matokeo Chanya

Dakika ya 38 Papy tshishimbi anapiga Shuti linapaa Juu

Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 28 Anamwekea Mpira mzuri Tshishimbi karibu kabisa na Goli Tshishimbi anapaisha kwa mara nyingine

Dakika ya 42 Yanga sasa Inacheza vizuri na Kutengeneza mashambulizi langoni mwa Welayta Dicha lakini Umakini unakosekana kwenye eneo la Mwisho.

Welayta Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 45 Haji Mwinyi anapewa kadi ya NJANO BAADA ya Kuonekana anachelewesha Muda wakati anarusha Mpira

Mpira ni Mapumziko katika uwanja wa Kimataifa wa Hawassa

Welayta Dicha 1 – 0 Yanga (Goli la dakika ya 2 ya Mchezo)

KIPINDI CHA PILI

Tayari Mbungi Imeanza

Dakika ya 46 Yusuph Mhilu anajaribu shuti kali mpira unagoma na kwenda Nje

Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 47 Obrey Chirwa anasababisha Kona kwa Kumgongesha Mchezaji wa Dicha.

Dakika ya 48 Hassan kessy anachonga Kona Nzuri lakini wachezaji wote wa Yanga wanashindwa Kuucheza.

Dakika ya 51 Yanaga wanafanya mabadiliko ya Kumtoa Kamusoko anaingia Said Juma Makapu, Gadiel Michael Naye anaonekana Uwanjani akiwa amechukua nafasi ya Haji Mwinyi mwenye kadi ya Njano

Dakika ya 56 Kipa wa Yanga Youthe Rostand Jehu anaonywa kwa Mdomo na Mwamuzi kutokana na Kuonekana kuchelewesha Mpira anapopiga Goal Kick

Dakika ya 57 Chirwa anapiga Kichwa Kinapaa Juu kidogo ya Lango la Dicha Ilikuwa Hatari

Dakika ya 60 Kelvin Yondani anapewa Kadi ya Njano kwa mchezo usio wa Kiungwana

Dakika ya 66 Anatoka Tshishimbi anaingia Emmanuel Martin, Tshishimbi anaonekana Kuumia

Dakika ya 75

Welayta Dicha 1 – 0 Yanga

Dakika ya 78 Mpira Unaonekana kubalance kwa Timu zote, lakini Matokeo yapo vile Vile wenyeji Welayta Dicha wakiongoza kwa bao 1 kwa 0

Dakika ya 80 Raphael Daudi ameumia anagoma kubebwa kwenye machela zao anatembea kutoka Nje Mwenyewe.

Dakika ya 84 Yanga wanaendelea kupoteza muda mdogo mdogo sasa Kipa Youthe Rostand Yupo chini akiashiria Ameumia.

Welayta Dicha 1 – 0 yanga

Dakika ya 88 sasa

Welayta Dicha 1 – 0 Yanga

Zimeongezwa dakika 3 za Nyongeza

Mabeki wa Yanga wanafanya makosa ya Kuuacha Mpira, Mshambuliaji wa Dicha anabaki na Kipa na Kupiga Nje

Mpira Umekwisha katika Uwanja wa Hawassa kwa Matokeo ya

Welayta Dicha 1 – 0 YANGA

Yanga wanafuzu kwa Matokeo ya Jumla ya Bao 2 kwa 1.

HONGERA YANGA, HONGERA TANZANIA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY