Matokeo Lipuli vs Simba 21 April 2018

Matokeo Lipuli vs Simba 21 April 2018

0

Matokeo Lipuli vs Simba 21 April 2018

Matokeo Kati ya Lipuli ya Mkoani Iringa dhidi ya Simba mechi ya Ligi Kuu INayochezwa uwanja wa Samora Mkoani Iringa.

>> Makundi kombe la Shirikisho barani Afrika <<

Timu zinasalimiana na Mgeni Rasmi.

Kabla ya mchezo kuanza Adam Salamba anakabidhiwa Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni moja na King’amuzi cha Azam Tv kama mchezaji bora wa Vodacom Premier League mwezi March.

Mechi imeanza katika uwanja wa Samora

Dakika ya 2 Simba wanapata mpira wa Adhabu mara baada ya Kichuya Kuchezewa madhambi

Anapiga Okwi mpira unakwenda Nje ya Lango

Dakika ya 7

Lipuli 0 – 0 Simba

Dakika ya 8 Salamba anaachia bakora Mpira Unapaa juu ya Lango la Simba

Dakika ya 10 Malimi Busungu anaamsha shangwe za Mashabiki baada ya Kupiga Chenga nzuri.

Dakika 15 Zimekatika

Lipuli 0 – 0 Simba

Dakika ya 17 Ilimiminwa nzuri na Nicolas Gyan lakini kipa wa Lipuli anapaa juu na Kudaka

Dakika ya 18 Seif Abdallah Karihe yupo chini mara baada kukutana na Chai kutoka kwa Juuko Murshid

Dakika ya 20 Mechi inaendelea

Lipuli 0 – 0 Simba

Dakika ya 22 Mpira wa Kuugusa Tu uliopigwa na John Bocco unashindwa kufikiwa na Shiza Kichuya na Asante Kwasi

Dakika 25

Lipuli 0 – 0 Simba

Dakika ya 28 Alichomoka Malimi Busungu Mshika kibendera ananyoosha kuonyesha ni Offside

Dakika ya 28 Shiza Kichuya anaachia Bakora kipa anatema hakuna mtu anauwahi na Kuudaka tena

Dakika 30

Lipuli 0 – 0 Simba

Dakika ya 31 Adam Salamba inainyanyua Samora kwa kufunga bao la Kwanza,Ulipigwa Mpira Mrefu Salamba akamgeuza Yusuph Mlipili na Kuujaza mpira nyavuni.

Lipuli 1 – 0 Simba

Dakika ya 34 Salamba tena anapaa hewani na Kupiga Kichwa Mpira unapaa, Lipuli wanachachamaa

Dakika ya 38 Walinzi wa Lipuli walifanya makosa Shiza Kichuya akapita na Mpira na Kuachia shuti ambalo Kipa wa Lipuli anaugusa na Kuwa Kona.

Dakika ya 39 Inapigwa Kona nyepesi kwa Kipa wa Lipuli anaudaka kirahisi.

Dakika ya 40

Lipuli 1 – 0 Simba

Okwi anaonekana si lolote kwa Walinzi wa Lipuli na anaonekana Laudit Mavugo akipasha.

Imeongezwa dakika 1 kufidia muda uliopotea Kipindi cha Kwanza

Lipuli wakiwa bado wanaongoza kwa bao 1 kwa 0

Kipyenga cha mwamuzi Hance Mabena kinapulizwa kuashiria kipindi cha Kwanza Kimemalizika

Lipuli 1 – 0 Simba (31′ Adam Salamba)

Ball Possession

Lipuli 51% – 49% Simba

KIPINDI CHA PILI

Timu zinarejea uwanjani kwaajili ya Kipindi cha Pili

Ametoka Juuko Murshid na Kuingia Laudit Mavugo

Mechi inaendelea Kipindi cha Pili

Dakika ya 45 Shomari Kapombe alijitwisha Kichwa kupitia krosi ya Kichuya lakini tayari alikuwa yupo Offside.

Dakika ya 46 Okwi anajaribu kwa mguu wa Kushoto mpira unakwenda Nje, Simba wameanza kwa kasi

Dakika ya 50 Aliwenda Vizuri Adam Salamba anapiga golini Simba wanakoswa koswa tena, shambulizi lilikuwa Hatari

Lipuli 1 – 0 Simba

Dakika ya 53 Shiza Kichuya anapiga shuti la chini chini lakini linakwenda pembeni ya lango

Dakika 60

Lipuli 1 – 0 Simba

Dakika ya 61 Shiza Kichuya anamweka Chini Saliboko wa Lipuli bado mambo ni magumu kwa Simba licha ya Kujitahidi kutengeneza nafasi

Dakika ya 63 Adam Salamba anamweka Salamba chini nje kidogo ya 18

Dakika ya 64 Mpira wa adhabu unaopigwa na LIPULI unakosa madhara

Dakika ya 65 Laudit Mavugo anasawazisha bao kwa mpira wa Kona

Lipuli 1 – 1 Simba

Dakika 70 Washabiki wa Simba waliokuwa KIMYA SASA WAMEAMKA Upya na wanashangilia kwa Nguvu

Lipuli 1 – 1 Simba

Dakika ya 79 Laudit Mavugo anakosa nafasi ya wazi akiwa yeye na Kipa

Zimesalia dakika 9 mchezo kumalizika matokeo yakiwa 1 kwa 1

Dakika ya 83 Okwi anawekwa chini nje kidogo ya Kumi na Nane, Ni Nafasi nzuri

Kipa anakua shujaa kwa Kuutoa na Kuwa Kona

Dakika ya 84 Kona ya Shiza Kichuya inadakwa na Kipa wa Lipuli Mohammed Yusuph

Dakika ya 87 alijaribu kupenya Mavugo lakini kipa anawahi kumdhibiti.

Lipuli 1 – 1 Simba (31’Adam Salamba, 65′ Laudit Mavugo )

Dakika 3 za Nyongeza zimeonyeshwa kufidia dakika zilizopotea

FULL TIME

Lipuli 1 – 1 Simba (31’Adam Salamba, 65′ Laudit Mavugo )

 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY