Kocha JULIO ataja anachofurahishwa kwenye Kikosi cha Yanga

Kocha JULIO ataja anachofurahishwa kwenye Kikosi cha Yanga

0

Kocha JULIO ataja anachofurahishwa kwenye Kikosi cha Yanga

JULIO ni kocha wa sasa wa Dodoma Fc ambao wanasikilizia rufaa yao ambayo wakishinda wanaweza kupanda Ligi Kuu, Julio pia Ni kocha wa zamani wa Simba, Coastal Union, Mwadui na amewahi Pia kucheza Simba.

Habari zaidi za Michezo Bonyeza>>  Hapa <<

Kocha huyo amesema moja kati ya Vitu vinavyomfurahisha kwenye Kikosi cha Yanga ni Falsafa ya Kutumia Wachezaji vijana ila amewataka kwa wakati kuachana na Suala la Ubingwa kwani anaona Simba wako Vizuri zaidi hivyo kama ni Kujipanga wajipange zaidi msimu Ujao kwani Vijana waliopo watawasaidia zaidi.

“Nadhani Yanga kwa sasa ingeachana na suala la ubingwa na kuendelea kuijenga timu yao kwa sababu imenifurahisha falsafa yao kutoa nafasi kwa vijana ambao naamini watakuja kuwa tishio katika msimu ujao kama ilivyofanya Simba miaka iliopita.”

Akiongea Kuhusu Ubingwa

“Unajua kila kitu mipango, Simba sasa hivi ni wakati wao, wapo vizuri na wanastahili kuendelea kushin­da kwa sababu kikosi chao kipo vizuri, kama wakiendelea na kasi hii kwa kushinda mechi mbili zijazo ikiwemo ya Yanga basi wa­takuwa mabingwa na hilo halina mjadala.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY