Yanga Yakimbiwa Botswana

  0

  Yanga Yakimbiwa Botswana

  Klabu ya Yanga ya Jijini Dar Es Salaam mara baada ya Kuingia mjini Gaborone Botswana wapinzani wao wameukimbia Mji Huo na kwenda kujiweka sawa kuelekea mchezo wa Jumamosi.

  Meneja wa Yanga Hafidh Saleh alisema taarifa za kuondoka na kutimkia mji mwingine wamezipata kutoka kwa wenyeji wao ambao ni Watanzania waishio nchini humo wenye mapenzi na Yanga.
  Saleh  msomaji wa Kwataunit.com alisema kwa mujibu wa taarifa ambazo wamezipata wenyeji wao, walishangazwa na ujio wao wa mapema nchini hapa ambapo wameshtushwa na ujio huo wakihofia mbinu zao kujulikana, hivyo wakaona waondoke mjini hapo.
  “Tangu tumefika hapa hatujawaona wapinzani wetu Rollers zaidi tulipata taarifa za wao kukimbia mji kutukwepa sisi wakihofia kuziona mbinu zao watakazozitumia.
  “Hatujui wamekwenda kuweka kambi yao hiyo kwenye mji gani, kikubwa tunashukuru wenyeji wetu waliotupokea baadhi wakiwemo Watanzania waishio hapa.
  “Kingine tunafurahia mapokezi mazuri tuliyoyapata kutoka kwa balozi wetu wa hapa nchini ambaye jana (juzi) tulikutana naye na kula chakula cha jioni na kubadilishana mawazo mbalimbali,”

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY