Yanga ndiyo timu pekee kuweka rekodi hii mzunguko wa 2 VPL

  0

  Yanga ndiyo timu pekee kuweka rekodi hii mzunguko wa 2 VPL

  Wakati Ligi Kuu ikishika Kasi na Mambo yakionekana kuwanogea Yanga kwa Ushindi wa Mfululizo kwenye Ligi Hiyo Yanga wameweka Rekodi mzunguko wa Pili.

  Kwasasa ukiwatoa Mtibwa Sugar timu nyingine zote zimeshacheza mechi 5 na Kuendelea kwenye mzunguko wa Pili.

  REKODI WALIYOIWEKA YANGA MZUNGUKO WA PILI

  Yanga Ndiyo timu pekee ambayo imefanikiwa kushinda ushindi wa Asilimia 100 Kwani katika mechi zake 5 mzunguko wa Pili imepata alama zote 15 huku kukiwa na Hakuna Timu nyingine Iliyofanya hivyo kwani Simba ambao ni wapinzani wa Yanga wametoa sare mbili katika mechi hizo Tano za Mwisho.

   

  Walianza na Lipuli wakawafunga 2 kwa 0 huko Iringa, Wakarejea Dar na kuwafunga Njombe Mji bao 4 kwa 0, Wakawafunga Maji MAJI Bao 4 kwa 1, Wakasafiri Mpaka Mtwara kucheza na Ndanda wakashinda bao 2 kwa 1 na Kisha Kucheza Na Kagera Sugar Taifa na kuwashushia Kipigo cha bao 3 kwa 0.

  WASHAMBULIAJI WANAFUNGA SIYO KITOTO

  Katika Mechi hizo 5 Yanga wanawastani mzuri pia wa Kufunga Magoli kwani wamefunga Jumla ya magoli 15 wastani wa Magoli matatu katika kila mechi.

  UKUTA HATARI

  Yanga msomaji wa Kwataunit.com katika michezo hiyo mitano Ukuta wake umeonekana kuwa Imara kwani katika mechi hizo tano za Mzunguko wa pili umeruhusu magoli mawili tu dhidi ya Maji Maji goli moja na Dhidi ya Ndanda.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY