Yanga mambo ni moto Botswana kama wapo Taifa tu kwa mipango hii

  0

  Yanga mambo ni moto Botswana kama wapo Taifa tu kwa mipango hii

  Wanachokifanya watanzania wanaoishi nchi ya Botswana na nchi za karibia na Botswana hakika Yanga watajisikia kama wapo nyumbani uwanja wa Taifa licha ya kuwa ukweli unabaki palepale kuwa mwenyeji atakuwa na washabiki wengi zaidi ya Yanga.

  Watanzania waliopo Botswana wao tayari wamejipanga kuwashangalia Yanga bila kujali tofauti za ushabiki wa Yanga na Simba kwani wamesema wanajali uzalendo na Utaifa kwanza.

  Acha waBongo wa Botswana, Hao Wasauzi siyo kwa Mapenzi haya.

  Watanzania wanaoishi Afrika Kusini nao wamejipanga vyema Kuungana na Wenzao wa Botswana kuwasapoti Yanga na tayari kulingana na Taarifa za Mpaka jana wapo ambao wameshaingia Botswana huku wengine wakitarajia Kuingia leo.

  Akizungumza na kituo cha Azam Tv jana mmoja ya watanzania waliopo Botswana Tayari alisema Watanzania wanaotokea Sauzi watakuwa wengi huku jambo la Kushangaza likiwa ni baadhi kutokea Umbali mrefu zaidi ya Kilomita 1700 kutoka Cape Town mpaka Gaborone kwenda Kuisapoti Yanga.

  Umbali Huu msomaji wa kwataunit.comĀ  unaweza Ukafananisha na Safari ya Kutoka Mbeya mpaka Bukoba kupitia njia Ya Biharamulo, Muleba mpaka Unaingia Bukoba na Bado ikawa hazijafika.

  Watanzania hao wanaoishi Nje nao wataungana na watanzania waliotokea Tanzania waliosafariri kwa njia ya basi kwenda Kuisapoti Yanga hivyo wakiungana mambo hayatakuwa mabaya sana kwa Yanga kwa Kujiona wapo wenyewe.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY