Yanga kuwakosa watatu wa kikosi cha kwanza mechi ijayo Kimataifa

  0

  Yanga kuwakosa watatu wa kikosi cha kwanza mechi ijayo Kimataifa

  Klabu Bingwa nchini Yanga ambayo ndiyo Timu pekee iliyobaki ikiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kimataifa mara baada ya timu nyingine zote Bara na Visiwani kutolewa.

  Kuelekea Mchezo ujao wa Kimataifa ambapo Yanga itacheza katika kombe la Shirikisho hatua ya Mtoano kabla ya kuingia Makundi Yanga itawakosa Beki Kelvin Yondani, Kiungo Papy Tshishimbi na Mshambuliaji Obrey Chirwa.

  Wachezaji hao watakosekana kutokana na kuwa na Kadi MBILIĀ  za Njano walizopata wakicheza dhidi ya Township Rollers Moja ya Nyumbani na ile ya Ugenini.

  Droo ya Kujua Yanga atacheza na nani msomaji wa Kwataunit.com itafanyika keshokutwa March 21 na Mechi hizo zinatarajiwa kucheza kati ya April 6 mpaka 8.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY