Yanga kucheza na kati ya timu hizi 15 Kimataifa Droo kufanyika leo

  0

  Yanga kucheza na kati ya timu hizi 15 Kimataifa Droo kufanyika leo

  Shirikisho la Soka Afrika (Caf), leo litachezesha droo jijini Cairo, Misri ambayo baadaye itatoa timu zitakazoshiriki hatua ya makundi.

  Yanga ambayo imeangukia katika michuano hiyo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Township Rollers ya Botswana, kuna uwezekano wa kukutano na moja kati ya vigogo wakali wakiwamo mabingwa wa Afrika 1998, Raja Casablanca ya Morocco.

  Mabingwa hao wa Bara, walikubali kipigo cha mabao 2-1 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kulazimishwa sare tasa nchini Botswana dhidi ya Township Rollers.

  Kwa matokeo hayo, Rollers yenyewe imetinga moja kwa moja hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

  Hivyo, sasa Yanga itamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16-Bora ya michuano hiyo, ambapo mbali na Raja Casablanca, pia zimo CR Belouizdad, USM Alger za Algeria, Al-Masry ya Misri, Djoliba ya Mali, Enyimba ya Nigeria, SuperSport United ya Afrika Kusini na Al-Hilal Al-Ubayyid ya Sudan.

  Aidha, mbali ya Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, wapinzani wengine wa timu hizo ni AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ASEC Mimosas, Williamsville AC za Ivory Coast, Saint George (Ethiopia), CF Mounana (Gabon), Aduana Stars (Ghana), Gor Mahia (Kenya) na UD Songo ya Msumbiji.

  Timu zingine ni MFM, Plateau United za Nigeria, Rayon Sports (Rwanda), Generation Foot (Senegal), Bidvest Wits (Afrika Kusini), Al-Hilal (Sudan) na Zanaco ya Zambia.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY