Yanga kuanza tizi leo,Fahamu watakaokosekana na Kivutio zaidi kwenye mazoezi ya leo

  0

  Yanga kuanza tizi leo,Fahamu watakaokosekana na Kivutio zaidi kwenye mazoezi ya leo

  Klabu Bingwa Nchini Dar Es Salaam Young Africans maarufu kama Yanga Leo wataanza mazoezi rasmi kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho kati yao dhidi ya Singida United.

  Mchezo huo utachezwa mwishoni mwa wiki hii, Yanga wamepeleka Kambi yao mjini Morogoro huku leo ikiwa ndiyo siku ya Kwanza ya mazoezi hayo.

  Wachezaji watakaokosekana kwenye mazoezi hayo.

  Yanga itaanza maandalizi ya mchezo huo na Singida United huku ikiwakosa wachezaji wake 5 ambao wapo Timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo dhidi ya Congo.

  Wachezaji hao ni Ramadhan Kabwili,Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Ibrahim AJibu.

  ATAKAYEKUWA KIVUTIO ZAIDI.

  Mchezaji ambaye anatarajiwa kuwa Kivutio zaidi ni Donald Ngoma ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na Kuwa majeruhi, Ngoma msomaji wa Kwataunit leo atafanya mazoezi na wenzake kwani Dr Bavu alithibitisha kuwa kwasasa yupo fiti asilimia 100 kuanza mazoezi na wenzzake.

   

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY