Wafahamu kwa Undani wapinzani wa Yanga Wolayta Dicha ya Ethiopia

  0

  Wafahamu kwa Undani wapinzani wa Yanga Wolayta Dicha ya Ethiopia

  Wolayta Dicha Fc au kama ambavyo huandikwa Wolaitta Dicha S.C. ) ni Klabu toka nchini Ethiopia ambayo ilianzishwa mwaka 2009 na Welayta Development  Association

  Mafanikio kwenye Ligi Kuu ya Ethiopia

  Baada ya timu hiyo kuanzishwa mwaka 2009 msomaji wa Kwataunit.com  ilianza kujiweka sawa mpaka msimu wa mwaka 2013/2014 ndipo walipoanza kushiriki ligi kuu ya nchini Ethiopia.

  Msimu wa 2016/2017 Timu hiyo ilionja mafanikio makubwa zaidi kwao kwani ndiyo mwaka ambao walinyanyua ndoo kama mabingwa wa Ethiopian Cup na Kuwafanya kuwa wawakilishi wa kombe la shirikisho Afrika.

  Kocha wao wa sasa anaitwa Zenebe Fisseha ambaye alijiunga na Timu hiyo mwaka 2017.

   

  Mafanikio Kimataifa

  Ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza kushiriki michuano ya KIMATAIFA Welayta Dicha katika mzunguko wa Kwanza walianza na Timu kutoka Zanzibar Zimamoto.

  Ambapo katika mchezo wa Kwanza uliochezwa huko Zanzibar mchezo uliisha kwa Sare ya bao 1 kwa 1 na Mchezo wa Marudiano Waethiopia hao wakashinda kwa bao 1 kwa 0 na Kufanya matokeo ya ujumla  msomaji wa Kwataunit kuwa 2 kwa 1.

  Baada ya Kuvuka hatua hiyo iliingia katika hatua ya 16 Bora ambapo walikutana uso kwa uso na Zamalek kutoka Misri ambao ni mabingwa wa zamani mara 5 wa klabu Bingwa Afrika ambapo matokeo ya mwanzo yalianza kwa Wolayta Dicha kushinda 2 kwa 1 Nyumbani.

  Katika mchezo wa Marudiano ukaisha kwa Matokeo kama hayo lakini safari hii Zamalek wakishinda hali iliyofanya mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Wolayta ilishinda kwa Penati 4 dhidi ya 3 za Zamalek na Zamalek kutoka kwenye mashindano.

  Hao ndiyo wapinzani wa yanga Kifupi hawana historia ndefu sana kwenye soka kutokana na kuwa Timu ILIYOANZISHWA miaka ya karibuni lakini mafanikio yake yameanza kuwafanya wapenzi wengi wa Soka kuanza kuwaangalia kwa jicho jingine.

  hasa pale ambapo walimtoa Bingwa mara tano wa Zamani klabu Bingwa Barani Afrika Zamalek hali ambayo haikutegemewa na watu wengi hasa kutokana na ugeni wa Timu hiyo kwenye mashindano ya kimataifa na Ukongwe wa Zamalek Kimataifa.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY