Wachezaji Yanga watuma Ujumbe Mzito, Mkwasa akubaliana nao.

  0

  Wachezaji Yanga watuma Ujumbe Mzito Mkwasa akubaliana nao.

  Nahodha wa Timu ya Yanga Nadir Haroub Cannavaro amesema kuwa licha ya Kuwa hali ya Uchumi ndani ya Klabu Bingwa Nchini Yanga ni mbaya amewaahidi washabiki wa Yanga wataendelea kupambania ubingwa huo lakini amewapa Ujumbe kuelekea mapambano hayo.

  Cannvaro amewaambia washabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga wajitokeze kwa Wingi uwanjani ili kuwasapoti lakini pia fedha zinazopatikana zitasaidia posho kwa wachezaji kwakuwa hali ya Kiuchumi siyo nzuri.

  Cannvaro msomaji wa kwataunit.com amesisitiza umuhimu wa washabiki kujitokeza uwanjani kuwasapoti timu inapocheza itawaongezea morali na kuwafanya wapambane zaidi.

  ” Tutapambana mpaka mwisho kuhakikisha tunatetea Ubingwa wetu lakini ukweli ni kwamba hali ya Kiuchumi ni ngumu, hivyo mashabiki wafike uwanjani na walipe kiingilio ili tupate Posho “

  Alisema Cannavaro.

  Mkwasa Abonga

  Naye katibu mkuu wa Timu Ya Yanga Boniface Mkwasa msomaji wa kwataunit.comĀ  alisema Mashabiki inabidi wabadilike na waanze kuingia uwanjani kwani kuingia kwao kwa wingi kutasaidia klabu kuweza kupata mapato na Kumudu Gharama za Uendeshaji.

  Hivyo ameendelea kusisitiza mashabiki wazime TV zao na waende uwanjani kwaajili ya kusapoti timu .

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY