Wachezaji wawili Stars wanaocheza nje kukosekana mechi dhidi ya Algeria

  0

  Wachezaji wawili Stars wanaocheza nje kukosekana mechi dhidi ya Algeria

  Kuelekea pambano kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania inayotarajia kusafiri kwenda mpaka Algeria kwaajili ya Mchezo wa Kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA Taarifa imetoka kuwa wawili wanaocheza nje watakosekana.

  Akizungumza na kwataunit.com meneja wa Timu ya Taifa Danny Msangi amesema wachezaji Thomas Ulimwengu na Farid Mussa watakosekana katika mchezo Huo kutokana na Sababu mbali mbali.

  Ulimwengu atakosekana kutokana na kukosa Visa kwani Passport yake ipo kwenye mamlaka ya ya kutafuta Vibali vya Kucheza kwenye klabu yake Mpya.

  Farid Mussa yeye klabu yake imembania kumpa Ruhusa ya kuondoka huko kwaajili ya kuungana na timu ya Taifa.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY