Usajili : Baada ya Yanga kutajwa kumtaka Mudathir Yahya,Yanga wafunguka haya..

  0

  Usajili : Baada ya Yanga kutajwa kumtaka Mudathir Yahya,Yanga wafunguka haya..

  Klabu ya Yanga ya Jijini Dar Es Salaam Tayari imeanza kutajwa kuwa ipo  katika mipango ya Kutaka Kumsajili aliyekuwa mchezaji wa Azam akicheza kwa Mkopo Singida United kwa Mkopo Mudathir Yahya Abbas.

  Mudathir Tayari ametajwa kumaliza Mkataba wake na Azam Fc na kwasasa ni mchezaji huru huku Azam wenyewe wakithibitisha Hilo kupitia kwa Msemaji wake Jaffar Iddi Maganga kuwa kwasasa Mudathir ni Mchezaji huru na anaruksa ya Kucheza timu yoyote.

  Yanga msomaji wa Kwataunit kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya Usaji Hussein Nyika amesema Kuwa hakuna ukweli juu ya Taarifa hizo na wao kama Yanga Mwalimu ndiye anayesajili mchezaji baada ya msimu kumalizika Mwalimu hupeleka mapendekezo yake kwa Uongozi.

  ” Baada ya msimu kumalizika mwalimu atatuletea ripoti lakini kwasasa hakuna mchezaji ambaye tumefanya naye mazungumzo,Hatuwezi kufanya usajili kwakuwa mchezaji yuko Free “

  Alisema Nyika.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY