Unaambiwa Yanga wakifanya mambo haya 2 Wolaita Dicha wanatoka

  0

  Unaambiwa Yanga wakifanya mambo haya 2 Wolaita Dicha wanatoka

  Katibu mkuu wa Timu ya Zimamoto kutoka visiwani Zanzibar Ally Usi Jongo amewaambia Yanga wanatakiwa kufanya mambo mawili tu kuwatoa Wolaita Dicha.

  Jongo msomaji wa Kwataunit.com amewaambia Yanga timu hiyo inasafu nzuri sana ya Ushambuliaji lakini hawana safu nzuri ya ulinzi hivyo wahakikishe wanamdhibiti mchezaji wao mmoja ambaye ndiye Tegemeo Kubwa kwa Timu Yao mchezaji anayeitwa Yakubu ambaye ni MuAngola anayecheza timu hiyo.

  “Wanayule mchezaji wao Muangola kama sikosei ambaye ndiye anaibeba Timu anaitwa Yakubu , Yanga wakiweza kumdhibiti huyu basi mechi imeisha wanasafu nzuri ya Ushambuliaji lakini safu ya Ulinzi siyo nzuri”

  Pia Jongo amesema Ili Yanga wawamalize Vizuri Wolaita Dicha basi inabidi mechi ianze saa tisa Alasiri.

  ” Kulingana na Hali ya hewa ya Ethiopia Mimi nawashauri Yanga mechi hiyo waianze saa tisa maana hali ya hewa ya Ethiopia ni baridi wakati kwetu joto ni kali “

  Zimamoto walitolewa na Wolaita Dicha kwa kufungwa Jumla ya goli 2 kwa 1, Mechi ya Kwanza Zanzibar ikiisha kwa sare ya bao 1 kwa 1 kisha kwenda Kufungwa 1 kwa 0 Ethiopia

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY