Township Rollers wataja aliyekuwa Kikwazo kwao mechi dhidi ya Yanga

  0

  Township Rollers wataja aliyekuwa Kikwazo kwao mechi dhidi ya Yanga

  Mechi ya Klabu Bingwa barani Afrika kati ya Township Rollers na Yanga ilimalizika kwa sare ya bila Kufungana huko Gaborone huku baadhi ya Wabotswana wakishindwa kuamini matokeo hayo kutokana na Matokeo ya awali.

  Wabotswana wengi waliamini Yanga angekufa bao za Kutosha kutokana na Matokeo ya awali Rollers kushinda bao 2 kwa 1 Ugenini.

  Lakini pia Wabotswana hao waliamini Yanga angekufa nyingi tu kama Ilivyokuwa kwa Al Merreikh ambaye alikufa 3 kwa 0 katika uwanja Huo.

  Baada ya mchezo huo msomaji wa kwataunit.comĀ  Mmoja ya wachezaji waliokuwa wasumbufu kutokana aina ya uchezaji wake Joel Mogorosi aliyekuwa na jezi namba 17 amemtaja Andrew Vicent kama ndiye aliyekuwa Kikwazo kwa Timu yao kupata matokeo dhidi ya Yanga.

  Mogorosi alisema Mabeki wa Kati walikuwa kikwazo Kelvin Yondani na Andrew Vicent huku akimsifia zaidi Andrew Vicent ambaye alioneka kutibua zaidi mipango yao kwa kucheza mipira Mingi kwa Miguu na Kichwa na kuonekana kisiki.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY