TFF yapangua tena ratiba kwa mchezo wa Yanga VPL saa 24 toka wapange ratiba Hiyo

  0

  TFF yapangua tena ratiba kwa mchezo wa Yanga VPL saa 24 toka wapange ratiba Hiyo

  Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania BARA VPL 2017/2018 Namba 199 kati ya Mbeya City na Yanga uliopangwa kufanyika Mei 1, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya umebadilishwa na sasa utapangiwa tarehe nyingine.

  Taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza kuwa uamuzi wa kuipangia tarehe nyingine mechi hiyo ni kukidhi matakwa ya Kanuni inayotaka nafasi kati ya mechi moja na nyingine isiwe chini ya angalau saa 72.

  Kwa mujibu wa ratiba, Yanga itakuwa na mechi dhidi ya Simba itakayofanyika Aprili 29, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo itakuwa ni vigumu kusafiri na kwenda kucheza huko Mbeya ndani ya saa 72.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY