Simba wampa dili kocha Al Masry

  0

  Simba wampa dili kocha Al Masry

  Mara tu baada ya Al Masry kuitoa Simba katika michuano ya Kimataifa kombe la Shirikisho barani Afrika kocha wa Al Masry Hossam Hassan amekula Dili.

  Hossam Hassan msomaji wa Kwataunit.com amepewa dili la Kuongeza mkataba wa Mwaka mmoja kuifundisha timu hiyo kutoka Port Said.

  Kama Simba wangeitoa Al Masry basi ingekuwa mwisho wa Hossam Hassan Kuifundisha Al Masry lakini ahadi ya Kuongeza mkataba ilikuwa ni kuhakikisha anaitoa Simba na kuipeleka timu 16 bora kitu ambacho amefanikisha na kusaini mkataba huo mpya.

  Kwa Tafsiri nyingine Simba ndiyo timu ambayo ilikuwa imeshikilia dili la Hossam Hassan kuacha au kuendelea kuifundisha Al Masry

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY