Papii Kocha aitaja Timu yake Kati ya Yanga na Simba

  0

  Papii Kocha aitaja Timu yake Kati ya Yanga na Simba

  Msanii wa muziki wa Dance nchini Papii kocha amefunguka juu ya Timu anazoshangilia ndani na Nje ya Nchi wakati akifanya mazunumzo kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm akiwa na baba yake Mzee Nguza Viking.

  Papii ambaye alikuwa jela kwa miaka 14 kabla ya kuachiwa kwa msamaha wa Rais amesema yeye kwa Tanzania ni shabiki wa Yanga .

  ” Mimi timu zote ni timu zangu lakini zaidi napenda Yanga “

  Upande wa Nje ya Nchi Papii msomaji wa kwataunit.com  amesema anaipenda Manchesteer City, Upande wa baba yake Papii Kocha mzee Nguza Viking yeye pia yupo Yanga na Nje ya Nchi ni Chelsea.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY