Abdi Banda aitaja moja ya mechi ngumu kuwahi kucheza na sababu

  0

  Abdi Banda aitaja moja ya mechi ngumu kuwahi kucheza na sababu

  Mtanzania Abdi Banda ameiongoza vyema timu yake ya Barioka Fc kupata Ushindi na kutinga hatua ya Robo Fainali Kombe la Nedbenk na kufanya timu hiyo kuungana na baadhi ya timu kama Kaizer Chief, Free State Warriors, Ubuntu Cape ambao nazo zimeshatangulia.

  Katika mchezo huo wa hatua ya 16 bora msomaji wa kwataunit.com Abdi Banda alicheza dakika zote 90 dhidi ya Sternberg United na kufanikiwa kushinda bao 2 kwa 0.

  Banda amesema pia hii ilikuwa moja kati ya mechi ngumu ambazo amewahi kucheza.

  • ”Moja ya michezo migumu ambayo nimecheza na huu naweza kusema ni mmoja wapo,jamaa wana washambuliaji wenye kasi na nguvu pia lakini tumecheza kwa umakini na tumeweza kuwazuia,molali ya kikosi chetu ni kubwa kwa kweli,” alisema Banda.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY