Nahodha Rollers ataja wachezaji Yanga walioambiwa wasiwape Upenyo mechi ya pili

  0

  Nahodha Rollers ataja wachezaji Yanga walioambiwa wasiwape Upenyo mechi ya Pili

  Nahodha wa timu ya Township Rollers Maano Ditshupo amesema kuwa mara baada ya mchezo wa Kwanza kati yao na Yanga benchi lao la Ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Nikola walikaa na wachezaji na Kufanya Tamthimini.

  Na katika mazungumzo yao waliwaweka wazi kuwa Ili wapate Kufuzu ni lazima kuwaangalia wachezaji wa Yanga waliokuwa hatari zaidi na Kuwapangia Mikakati.

  Katika mazungumzo hayo msomaji wa Kwataunit  wachezaji ambao waliwekwa kwenye kitimoto ni Ibrahim Ajibu na Papy Tshishimbi ambao kulingana na Maelezo ya Maano Ditshupo walijipanga kuhakikisha hawatawasumbua kama ilivyokuwa katika mchezo wa Kwanza.

  Hata hivyo akili ya George Lwandamina ni kama ilisikia mazungumzo yao kwani katika mchezo huo alimwanzisha nje Ibrahim Ajibu ambaye aliingia dakika ya 70.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY