Mkutano Mkuu Yanga Kufanyika Mei 5 2018

  0

  Mkutano Mkuu Yanga Kufanyika Mei 5 2018

  KATIBU Mkuu wa Young Africans  Sports Club Charles Boniface Mkwasa ametangaza siku maalumu ambayo klabu  itafanya mkutano mkuu wa wanachama wote,kujadili masuala mbalimbali muhimu ya maendeleo.

  Muda mfupi uliopita Mkwasa ameiambia  www.yangasc.co.tz kuwa wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada zao mapema kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.

  Mkutano utafanyika Mei 5/2018 hapa jijini Dar es Salaam, wanachama wenye kadi aina zote mbili wataruhusiwa kuingia ukumbuni, kwa maana ya wale wenye kadi za zamani na hizi zinazotolewa sasa kupitia benki ya posta.

   

  Akiendelea zaidi Mkwasa amesema kuwa, kupitia kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika  jumapili iliyopita, kamati   imeridhia kufanyika kwa Mkutano huo, na kuomba wanachama kujindaa kwa ajenda ambazo zitatangazwa baaadae.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY