Mganga aliyesababisha Mvua asema Simba inaweza Kushinda ugenini Ikifanya Hivi

  0

  Mganga aliyesababisha Mvua asema Simba inaweza Kushinda ugenini Ikifanya Hivi

  Bwana Eeeh watu na Teknolojia zao asikuambie Mtu Mganga mmoja kutoka Mkoa wa Rukwa huko mjini Sumbawanga anayejulikana kama Dr. Kata Ushanga amesema kuwa yeye ndiye aliyesababisha mvua katika uwanja wa Taifa Simba ikicheza dhidi ya Al Masry.

  Dr Kata Ushanga Akizungumza katika kipindi cha Michezo cha Clouds Fm  amesema kama Mvua isingekatika basi Mwarabu alikuwa anakufa goli 3 lakini kilichoharibu ilikuwa ni kukatika Umeme, Amesema yeye alileta mvua kama kitendo cha Kubariki uwanja na siyo kuwavurugia Simba ila umeme ndiyo uliharibu kila kitu.

  Dr KataUshanga anadai alikuwa uwanjani katika mchezo huo na alianza maandalizi mapema ikiwa ni kwa mapenzi yake kwa nchi kwani hakutaka kushirikiana na uongozi.

  AMEWAHI KUFANYA KAZI KWAAJILI YA STARS

  Mganga huyo msomaji wa Kwataunit.com  amesema aliwahi kufanya kazi kwenye mchezo kati ya Chad na Tanzania mchezo uliofanyika huko Chad na Stars ilishinda kwa bao 2 kwa 1 akifanya kazi hiyo mara baada ya Kugundua mkuu wa msafara wa Stars alikuwa anatokea Mkoa wa Rukwa.

  WAARABU WANAWEZA KUFUNGWA KWAO.

  Dr Kata Ushanga amesema Mwaabu anaweza kufungwa hata huko Uarabuni kama Simba wako tayari basi wafanye kazi kwani yeye ni Mtaalamu ambaye amekuwa anauwezo wa kutuma mvua hata Ulaya na Ikafanya yake.

  ” Mimi niko tayari kama wako tayari kwa kazi hiyo tufanye kazi nitelemshe majeshi yangu tutaishangaza dunia, Mimi mvua ni kawaida yangu kuna ile ya Live kuna ile ya kutembea kimya kimya nyingine huwa tunazishika hata kwa Mkono Tu tunazo za aina nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi hata kama uko ulaya Tunatuma tu “

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY