Mfahamu Straika aliyemfanya Mlipili atafute video zake Youtube kabla ili kumkaba

  0

  Mfahamu Straika aliyemfanya Mlipili atafute video zake Youtube kabla ili kumkaba

  Beki wa Kati wa Timu ya Simba Yusuph Mlipili ambaye alijiunga Na Simba Msimu Huu akitokea klabu ya Toto Africa ya jijini Mwanza lakini pia akiwa aliwahi kucheza katika timu ya African Lyon amefunga Straika ambaye amewahi kumuogopesha kiasi cha kutafuta Clip zake za Video Youtube kabla ya kukutana naye.

  Mlipili msomaji wa Kwataunit  amemtaja Straika wa Al Masry Aristid Bance kuwa ni moja ya Mastraika ambao walimfanya ajiandae isivyokawaida yake.

  ” Mechi ya Al Masry kuna mtu yule Bance¬† nilikuwa namhofia niliingia mpaka Youtube ili kumuangalia kwanza ukiangalia uzito wangu na wake ni tofauti na hata maisha yao na yetu ni tofauti “

  Katika hatua Nyingine Mlipili ameweka wazi kuwa kati ya Messi na Cristian Ronaldo anamkubali zaidi Ronaldo kutokana na mambo yake uwanjani na hata mwili wake umekaa kisoka.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY