Mechi ya Simba na Yanga baada ya Panga Pangua TFF yapanga ichezwe tarehe hii

  0

  Mechi ya Simba na Yanga baada ya Panga Nipangue sasa kuchezwa tarehe hii

  Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema mechi ya watani ya jadi kati ya Simba na Yanga utachezwa Aprili 29, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Mechi hiyo ya watani wa jadi awali ilikuwa ichezwe Aprili 7, lakini baada ya Yanga kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa na kuondokea Kombe la Shirikisho Afrika katika tarehe hizo itakuwa na mechi ya kwanza ya mtoano dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia.

  Simba inaongoza Ligi Kuu kwa tofauti ya mabao na Yanga baada ya kufungana kwa pointi 46, hivyo kusogezwa mbele kwa mechi baina yao inafanya mbio za ubingwa kuwa wazi zaidi kwa timu hizo.
  Yanga na Simba zitakapokutana Aprili 29, kila timu itakuwa imebakiza mechi tano kabla ya kumaliza msimu.

  Hata hivyo mechi hiyo ya Aprili 29, italazimisha kusogezwa mbele kwa mechi kati ya Lipuli na Simba iliyokuwa ifanyikea Aprili 28, kwenye Uwanja wa Samora, Iringa pamoja na ile ya Prisons dhidi ya Yanga ilikuwa ichezwe Aprili 29, kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY