Mchezaji bora wa Mwezi February ligi kuu VPL huyu hapa

  0

  Mchezaji bora wa Mwezi February ligi kuu VPL huyu hapa

  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Papy Kabamba Tshishimbi kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mwezi Februari huku akiwabwaga Pius Buswita na Emmanuel Okwi.

  TFF ilitangaza tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi huu wakati Msemaji wa shirikisho hilo ali[pokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne.

  Tshishimbi ambaye ni raia wa Congo, amesafiri na kikosi cha timu yake kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Township Rollers.

  Kiungo huyo wa Yanga, timu yake imefikisha pointi 46 kwenye msimamo wa Ligi Kuu sawa na Simba iliyopo kileleni wakiwa na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY