Mchezaji aliyekuwa Gumzo zaidi wa Simba huko Misri baada ya Sare na Al Masry

  0

  Mchezaji aliyekuwa Gumzo zaidi wa Simba huko Misri baada ya Sare Al Masry vs Simba

  Mara baada ya Mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Al Masry na Simba kumalizika kwa Simba kuwalazimisha sare Waarabu sare ya bila kufungana kuna mchezaji amekuwa Gumzo nchini Misri.

  Katika Mchezo huo  msomaji wa kwataunit.com  Waarabu walionekana kulisakama vilivyo lango la Yanga hasa katika kipindi cha Kwanza kikwazo kilikuwa kwa Safu ya Ulinzi ya Simba.

  Lakini Waarabu wa huko Misri walipagawa Vilivyo na uwezo wa Golikipa Aishi Manula ambaye katika mnchezo huo alionyesha uwezo wa Hali ya Juu kwa kuokoa mipira mingi iliyokuwa ikielekea langoni Mwake.

  Kucheza vizuri zaidi kwa Aishi Manula ambaye alionekana kuwa makini sana Langoni kuliwafanya baadhi ya washabiki wengi wa Al Masry kumuona  Kikwazo kwa washambuliaji wao kufunga na pia Manula ndiye aliyekuwa mchezaji bora kwa upande wa Simba

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY