Matokeo Tanzania/Taifa Stars vs Congo 27 March 2018

  0

  Matokeo Tanzania/Taifa Stars vs Congo 27 March 2018

  Mechi Imeanza katika uwanja wa Taifa

  Mashabiki waliofika uwanjani wanaonekana kuwashangilia kwa nguvu Stars wanaposonga Mbele

  Dakika ya 4 Kichuya anapiga Shuti linapaa ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Stars kupata goli kama Kichuya angekuwa Mtulivu, Bado 0 kwa 0

  Dakika ya 7 Abdi Banda anamwangusha Mubele Ndombe aliyekuwa akielekea langoni mwa Stars ni Faulo, Manula anapanga Ukuta wake

  Walinzi wa Stars wanacheza mpira wa Faulo na kuokoa kuutoa Langoni mwao

  Dakika ya 10

  Stars 0 – 0 Congo

  Mpira umetulia kwa dakika hizi 10 mpaka 15 na timu zote zikionekana kutengeneza nafasi lakini bado matokeo ni 0 kwa 0

  18′ Mohmmed Issa Banka anaonekana kujiamini na Kucheza Vizuri anamchukua Beki wa Congo vizuri lakini mpira unatoka Nje, Bado ni 0 kwa 0

  Dakika 20 za Kipindi cha Kwanza zimekatika katika uwanja wa Taifa bado ni matokeo tasa kwa timu zote

  Dakika ya 21 Congo wanapata Kona lakini inakuwa haina madhara kwa Stars

   

  Dakika ya 22 Woyoo woyoo woyoo inasikika kutoka kwa mashabiki walioingia uwanjani kuisapoti Taifa Stars

  Dakika ya 25 Gadiel Michael anaachia shuti kali kipa wa DRC Congo  Matampi anaitoa na Kuwa Kona kwa upande wa Stars kona ambayo inashindwa kuzaa matunda kwa Tanzania

  Abdi Banda katika dakika ya 25 anapewa kadi ya Njano baada ya kumwangusha mchezaji wa Congo

  Dakika ya 30 Samatta anaondoka na Mpira kwa kasi lakini anapiga Krosi mbovu, Bado 0 kwa 0 msomaji wa Kwataunit.com

  Zinapigwa Pasi Fupi fupi kadhaa na Stars Kapombe anapiga KROSI beki anatoa nje  inakuwa Kona

  Dakika ya 37 Wanacheza kona mbili mfululizo lakini hazina Matokeo chanya kwa Stars

  Dakika  ya 44 Shiza Kichuya anapiga Shuti Hafifu kipa anadaka bado ni 0 kwa 0

  Almanusra Shomari achome tena Kibanda wakati akirudisha mpira kwa kichwa golini lakini Kipa Manula anawahi kuucheza mpira

  Dakika 45 za Kipindi cha Kwanza katika uwanja wa Taifa mechi ya kirafiki kati ya Tanzania na Congo zimemalizika kwa sare ya bila Kufungana.

  Timu zote zimecheza kwa nidhamu kubwa huku mipango ikionekana kukwama kwa timu zote ndiyo maana bado 0 kwa 0

  Ball Possession kwa Kipindi cha Kwanza

  Tanzania 51% wakati Congo 49%

  KIPINDI CHA PILI KIMEANZA

  Taifa Stars 0 – 0 Congo

  Dakika ya 47 Samatta anawekwa Chini inakuwa Faulo

  Stars wanacheza lakini hakuna Kitu bado 0 kwa 0

  Dakika ya 48 Msuva anasukumwa kwenye eneo la penati lakini mwamuzi Elly Sasi anakataa kuweka Tuta

   

  Dakika ya 51 Msuva anakokota Mpira na kupiga Shuti kali linalogusa nyavu za Pembeni na kuwa Goal Kick

  Dakika ya 55 Mara baada ya Ibrahim Ajibu Kuinuka na Kuanza kufanya mazoezi mashabiki wanapiga Kelele za Kumshangilia

  Dakika ya 60 Ibrahim Ajibu anaingia Anapishwa na Mo Issa Banka

  61′ Ibrahim Ajibu anapiga shuti linapaa

  62 ‘ Pasi inatoka kwa Ajibu inakwenda kwa Gadiel, Gadiel anapiga kwa Msuva na Msuva anaweka goli lakini inakuwa tayari ni Offside

  Dakika ya 68 Bado 0 kwa 0

  Dakika ya 71 Gadiel Michael anaumia mara baada ya kuwa anaokoa Mpira Uliokuwa ukielekea Langoni mwa Taifa Stars

  Dakika ya 74 Mpira Mrefu unapigwa na Kelvin Yondani kwa Msuva, Msuva anakokota anaupiga kwa Kichuya, Kichuya anapiga Krosi, Ajibu na SAMATTA wanapanda hewani na Samatta aliyekuwa mbele anafunga bao kwa Kichwa.

  Tanzania 1 – 0 Congo

  Dakika ya 84 Ajibu  alimtanguliza Beki wa Congo lakini anawekwa Chini, Beki anapewa Kadi ya Njano

  Dakika ya 86 Shiza Ramadhan Kichuya anaweka bao kwa Shuti kali nje ya kumi na nane, Pasi ilitokea kwa Msuva aliyekokota akaiweka kwa Samatta, Samatta akaicheza kwa Kichuya ambaye anaweka Goli safi

  Stars 2 – 0 Congo

  87’ Shiza Kichuya anatoka anaingia Rashid Mandawa

  Zimebaki dakika nne za Nyongeza bado Stars wanaongoza kwa bao 2 kwa 0

  Msuva anatoka anaingia Yahya Zayd

  Dakika 90 zimemalizika kwa Tanzania Kushinda ba0 2 kwa 0.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY