Matokeo Algeria vs Tanzania 22 March 2018

  0

  Matokeo Algeria vs Tanzania 22 March 2018

  Mechi imeanza

  Dakika ya 12 Algeria wanapata bao la Kuongoza

  14′ Samatta anakosa Goli anapiga pembeni kipa anaokoa kwa Mguu

  Dakika ya 17 Bado Algeria wako mbele kwa bao Moja

  Dakika ya 20 Simon Msuva akitumia Kichwa chake Vizuri kwa Kona Iliyopigwa na Shiza Kichuya anasawazisha bao nakufanya matokeo kuwa 1 kwa 1.

  Dakika 25 zimekatika bado matokeo ni 1 kwa Algeria na 1 kwa Tanzania wakianza Algeria kabla ya Stars Kusawazisha kupitia kwa Simon Msuva

  Dakika 30 zimekatika bado 1 kwa 1

  Washabiki wa Algeria wanaonekana kuanza Kuimba wimbo wa pamoja KUWASAPOTI wachezaji wao lakini Stars wanaposhika Mpira filimbi na Miluzi Inasikika.

  37′ Bado 1 kwa 1

  Dakika 40 zimeshakatika zimebaki 5 kumaliza kipindi cha Kwanza Mechi ikiwa  Algeria Wenyeji 1 Taifa Stars 1

  Dakika ya 43 Shomari Kapombe anajifunga goli kwa kichwa akijitahidi kuokoa Mpira

  Algeria 2 – 1 Tanzania / Taifa Stars

  Mpira ni Mapumziko Algeria ambao ni wenyeji wanaongoza kwa bao 2 dhidi ya 1 la Tanzania, Algeria walianza kufunga bao dakika ya 12, Simon Msuva akachomoa goli hilo kwa Kichwa, Kisha Algeria wakaongeza bao mara baada ya Mlinzi Shomari Kapombe Kujifunga kwa Kichwa akijitahidi kuokoa.

  KIPINDI CHA PILI

  Kipindi cha Pili kimeanza

  Dakika ya 50 sasa bado ALgeria 2 na Tanzania 1.

  Dakika ya 53 Algeria wanapata bao la 3, Algeria 3 – 1 Tanzania

  dakika ya 55 Samatta anaangushwa kwenye eneo la 18 lakini Refa anapeta

  Dakika ya 64 bado Stars iko nyuma kwa bao 3 kwa 1

  66′ Gadiel Michael anaachia Mkwaju kipa anaupalaza na unagonga mwamba, Mudathir anarudishia Kipa anatoa tena na Kuwa Kona

  dakika ya 70 Bado ni 3 kwa 1

  74′ Kichuya anatoka anaingia Mo Banka, Bado Algeria 3 – 1 Tanzania

  79′ Baada ya Kuwalamba chenga mabeki watatu wa Stars mshambuliaji wa Algeria anafunga bao la 4 kwa Algeria.

  Algeria 4 – 1 Tanzania

  87 Rashid Mandawa anaingia kuchukua nafasi  ya mudathir Yahya Abbas

  Mechi ya Kirafiki kati ya Timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars waliokuwa ugenini kucheza dhidi ya Algeria umemalizika kwa Algeria kushinda kwa jumla ya bao 4 kwa 1

  Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY