Matokeo Al Masry vs Simba leo March 17, 2018

  0

  Matokeo Al Masry vs Simba leo March 17, 2018

  Matokeo Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Al masry ambao ni wenyeji wa Mchezo wakiikaribisha Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania Katika michuano hiyo.

  Kwa matokeo haya Simba inaondolewa kwenye michuano hiyo kwa kuwa tu Al Masry walipata goli ugenini wakati wa sare ya bao 2 kwa 2.

  FULL TIME : Al Masry 0 – 0 simba

  dakika 90 zimeisha bado za nyongeza , ni 0 kwa 0

  73′ Anatoka James Kotei anaingia Shiza Kichuya

  Mabeki wa Simba wanaonyesha wako makini na Bance kwani wanamweka mtu kati  mabeki wa watatu

  dakika ya 70 bado viduara vimetawala kwa timu zote

  68′ James Kotei yupo chini akitibiwa baada ya kuumia

  65′ Anaingia Mavugo anatoka Yusuph Mlipili

  60′ Al masry 0 – 0 Simba

  licha ya al masry kupata mipira kadhaa ya adhabu karibu na 18 bado Simba wamekuwa salama, dakika ya 60 ni bila kwa bila

  Dakika ya 50 Bado mambo yamekaza pande zote

  kipindi cha pili kimeanza bado 0 kwa 0

  Kipindi cha Kwanza Kimemalizika Simba wameonekana kupaki basi muda mrefu ikiwa ni mbinu ya Kutoruhusu Bao na wamekuwa wakipata Mpira wanacheza kwa kasi.

  HT Al Masry 0 – 0 Simba

  45+ Asante Kwasi anapewa kadi ya njano

  Dakika ya 40 Yusuph Mlipili anamweka Chini Leissa nje kidogo ya 18 na kuwa Faulo

  dakika ya 35 port said bado mambo magumu kwa timu zote

  Kuna Shughuli uwanjani kati ya Bance na Beki Juuko Murshid acha kabisa

  30′ Al Masry 0 – 0 Simba

  Upande wa Nicolas Gyan anayecheza kama beki wa Kulia Unaonekana kuruhusu krosi nyingi ambazo Aishi Manula ameonyesha yuko Vizuri kuzicheza

  25′ Al masry 0 – 0 Simba

  Simba wanaonekana wakijilinda katika hali ya nidhamu huku wanapopata mpira wanaonekana kucheza kwa spidi kiasi.

  19′ manula yupo chini akitibiwa mara baada ya kuumia kwenye harakati za kuokoa mpira

  Dakika ya 12 Aristid Bance anaingia kuchukua nafasi ya mchezaji aliyeumia upande wa Al masry

  dakika ya 1o Port said bado ni 0 kwa 0

  dakika ya 6 Al masry wanapata faulo karibu na 18  inayochezwa na ukuta wa Simba unokoa

  dakika ya 5 bado 0 kwa 0

  Mechi Imeanza Port Said bado Al Masry 0 – 0 Simba

   

  > Kuzipata habari zetu kila wakati kwa haraka Like Ukurasa wetu wa Facebook Bonyeza hapa <

   

   

  Kikosi cha Simba dhidi ya Al Masry hiki Hapa

  Kikosi cha Simba Kinachoanza dhidi ya Al Masry katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika Mchezo ukiwa ni wa marudiano baada ya ule wa kwanza Kuisha kwa sare ya bao 2 kwa 2 Dar Es Salaam.

   

  1. Aishi Manula
  2. Nicolas Gyan
  3. Asante Kwasi
  4. Erasto Nyoni
  5. Juuko Murshid
  6. Mkude Jonas
  7. James Kotei
  8. Kapombe Shomari
  9. John Bocco
  10. Emmanuel Okwi
  11. Said Ndemla

  Wachezaji wa Akiba

  1. Said Mohammed
  2. Mohammed Hussein
  3. Paul Bukaba
  4. Shiza Kichuya
  5. Mzamiru Yassin
  6. Laudit Mavugo
  7. Mwinyi Kazimoto

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY