Masoud Djuma : Msitegemee kwaona wachezaji hawa mechi ijayo

  0

  Masoud Djuma : Msitegemee kwaona wachezaji hawa mechi ijayo

  Kocha Msaidizi wa Timu ya Simba raia wa Burundi Masoud Djuma amesema washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba wasitegemee kuwaona wachezaji ambao wamerejea kutoka kuwa majeruhi.

  Djuma msomaji wa Kwataunit.com amesema kwasasa wamejipanga kutotumia mchezaji aliyetoka kwenye majeraha mpaka apone kabisa.

  Amesema kuwachezesha wachezaji ambao wametoka kwenye majeraha kumekuwa kukiwasababisha wachezaji kutokupona haraka kutokana na kujitonesha mara kwa mara.

  ” hatutaki kuwachezesha wachezaji waliotoka kwenye majeraha kwani kufanya hivyo kumekuwa kunawarejesha tena kwenye hali hiyo, Ni bora tusubiri mchezaji apone kabisa ndipo tuanze Kumtumia ” alisema Masoud Djuma.

  Kwa Hali hiyo wachezaji kama Haruna Niyonzima, Salim Mbonde na John Bocco huenda bado wakaendelea kukosekana kwenye Kikosi cha Simba.

  Simba kwasasa wanajiandaa na Mchezo kati yao dhidi ya Njombe Mji April 3 2018 katika mchezo utakaochezwa huko mjini Njombe.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY