Maoni ya Mohammed Mwameja kuhusu uwezo wa Kabwili na Goli alilofungwa na Rollers

  0

  Maoni ya Mohammed Mwameja kuhusu uwezo wa Kabwili na Goli alilofungwa na Rollers

  Mara baada ya Yanga Kufungwa Goli la Mbali na Mchezaji Wa Township Rollers Lemponye dakika ya 11 Kuna baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama  wa Yanga walianza kuona kama ulikuwa ni uzembe wa Golikipa Ramadhan Kabwili.

  Baadhi walisema kwa Mpira kama ule angekuwepo Youthe Rostand basi kusingekuwa na Goli katika Lango la Yanga lakini kila mtu na Maoni na Mtazamo wake.

  Lakini Kipa wa zamani wa Timu ya Taifa ya TANZANIA na Kipa wa zamani wa  Simba Mohammed Mwameja “Tanzania One” Moja kati ya Makipa bora kuwahi kutokea Nchini Tanzania msomaji wa Kwataunit kama ulikuwa Huijui Hii ametoa maoni yake Kuhusiana na Uwezo wa Kabwili na Goli alilofungwa.

  Mwameja ambaye kwasasa alishastaafu kucheza soka amesema Goli akilofungwa Ramadhani Kabwili ni Goli la kawaida kabisa katika soka maana Movement za goli zilianzia Mbali na Yanga hawapaswi kumkatia tamaa golikipa Huyo.

   

  Mohammed Mwameja amesema Ramadhani Kabwili ni Kipa Mzuri kama akiendelea kukuzwa na atakuja kuisaidia Yanga na Taifa kwa Ujumla.

  “ goli alilofungwa Ramadhani Kabwili ni la kawaida . Ni goli ambalo movements zilianzia mbali hivyo Yanga isimkatie tamaa kijana huyo. Ni golikipa mzuri akiendelea kukuzwa kwa Yanga na taifa . Binafsi namuamini sana” 

  Alimaliza Mohamedi Mwameja

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY