Manara akumbusha makipa wawili ambao wamewahi kufunga ndani ya dakika 90 mechi ya Watani

  0

  Manara akumbusha makipa wawili ambao wamewahi kufunga ndani ya dakika 90 mechi ya Watani

  Haji Manara ambaye amekuwa akichangamsha  Genge kwenye mtandao wake wa Kijamii wa Instagram amekumbusha makipa wawili ambao wamewahi kufunga magoli kwenye mechi za watani wa Jadi Simba na Yanga.

  Haji Manara kama unavyojua yeye na Simba Humtoi amewataja makipa hao kuwa ni Iddi Pazi wa Simba na Juma Kaseja naye kutoka Simba,

  Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Manara msomaji wa Kwataunit  ameandika Ujumbe Huu.

  “Najua hujui ila leo ntakujuza ili upate kujua..Iddi Pazi ‘father ‘Na Juma kaseja ndio makipa pekee nchini kufunga ktk dak tisini za mchezo kwenye derby ya DSM..Pazi alifunga ktk sare baina ya Simba na Yanga 1984 iloisha 1-1 Na kaseja alifunga ktk ushindi mkubwa zaid ktk karne hii kwa watani hao, 5 kwa Simba na Yai kwa Yanga @official_juma_kaseja”

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY