Kwa Hili Sasa ni rahisi Kichuya kutua Tp Mazembe.. Sababu hizi hapa

  0

  Kwa Hili Sasa ni rahisi Kichuya kutua Tp Mazembe.. Sababu hizi hapa

  Jana vyombo vingi vya Habari nchini msomaji wa Kwataunit Viliripoti taarifa ya Shiza Kichuya kuwa katika rada za mabingwa mara kadhaa wa Afrika katika michuano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho kwa Vilabu barani Afrika Tp Mazembe.

  Taarifa zilidai kuwa Tp Mazembe tayari wamejipanga kuhakikisha wanaipata Saini ya Winga machachari na hatari Shiza Kichuya ambaye kwa msimu  huu amekuwa na Sifa ya kufunga na Kuassist kiasi cha Kuwa ndiye mchezaji mwenye assist nyingi zaidi ligi kuu mpaka sasa.

  Kichuya kwenda Tp Mazembe itakuwa rahisi zaidi kama tu kumsukuma Mlevi kwani Mkataba wa Simba na Kichuya unaelekea mwishoni.

  Mkataba wa Kichuya unaelekea kuisha na Utaisha mwishoni mwa Msimu huu hali ambayo itamfanya Kichuya kuwa mchezaji huru na kama mazungumzo yatakuwa kati ya Kichuya na Mazembe na Siyo Mazembe na Simba kama Kichuya angekuwa bado anamkataba.

  >> SOMA HABARI ZOTE ZA  SIMBA HAPA <<

  Urahisi zaidi wa Kichuya kwenda Mazembe unaweza ukaletwa na msimamo wa Kichuya ambao amekuwa nao kwa siku za Karibuni kwani Taarifa za Kuaminika zinadai kuwa winga huyo amegoma kuongeza mkataba ndani ya Simba mpaka msimu utakapomalizika.

  Kama Kichuya hataongeza mkataba basi atakuwa mchezaji huru na hata gharama zitapungua kwa Tp Mazembe kumsaini kwani Makubaliano yatakuwa baina ya Mazembe na Kichuya na Siyo Kichuya, Mazembe na Simba

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY