Kocha Rollers ataja mchezaji aliyewasumbua Yanga aahidi kuhakisha wanamsajili

  0

  Kocha Rollers ataja mchezaji aliyewasumbua Yanga aahidi kuhakisha wanamsajili

  Kocha Mkuu wa Mabingwa wa soka nchini Botswana Timu ya Township Rollers Nikola Kavazonic ambaye March 6 2018 kikosi chake kilipata Ushindi wa bao 2 kwa 1 kikicheza na Mabingwa wa soka nchini Yanga uwanja wa Taifa Dar Es Salaam amemtaja mchezaji aliyewasumbua zaidi kwenye mchezo huo.

  Nikola ambaye alijinasibu kabla ya mchezo huo kuwa analijua  vizuri soka la Afrika amesema mchezaji Papy Kabamba Tshishimbi ndiye aliyekuwa hatari zaidi kwa timu yake eneo la katikati ya uwanja.

  Kocha huyo amesema Tshishimbi aliwasumbua sana viungo wake hasa katika kipindi cha Kwanza, Katika Mchezo huo Tshishimbi ndiye aliyetoa pia pasi ya Goli naye akipokea pasi kutoka kwa Pius Buswita Tshishimbi akiipokea na Kuipiga moja kwa moja kwa Chirwa aliyeweka Mpira nyavuni.

  NIKOLA –  NITAHAKIKISHA ANAJIUNGA NA ROLLERS.

  Kutokana na kuona uwezo wake kocha huyo amekiri na kusema Tshishimbi anakipaji kikubwa sana na atahakikisha anawashawishi viongozi wa Rollers kuhakikisha ananasa saini ya Nyota huyo wa Yanga.

  Kocha huyo amesema wanataka washinde kwanza mchezo unaofuata na kisha wakae mezani na Yanga ili wamalizane kuhusiana na Tshishimbi kwani Kama watafuzu hatua ya Makundi anaona kabisa Tshishimbi atawasaidia mno kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

  FEDHA SIYO TATIZO KWA ROLLERS

  Kama kocha huyo  msomaji wa Kwataunit atalifikisha suala la Kumwitaji Tshishimbi basi ni wazi Tshishimbi lazima atatua kwao kwani kwao fedha siyo Tatizo kabisa kwasasa labda Yanga ndiyo waamue kumkatalia Tshishimbi kwani Unaambiwa Rollers kwasasa ni moja kati ya timu zilizo vizuri kiuchumi barani Afrika.

   

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY