Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Stand United leo

  0

  Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Stand United leo

  Hiki ni kikosi cha Utabiri cha Yanga kinachoweza kuanza Leo dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi kuu Soka ya Tanzania Bara  VPL

  GOLINI : Bila shaka unaweza Kuanza Kipa Youthe  Rostand ambaye anapokuwa mzima asilimia 100 amekuwa akiaminiwa zaidi na Benchi la ufundi la klabu ya Yanga chini ya kocha Mkuu George ” Chicken” Lwandamina.

  Mabeki wa pembeni: Kuna mambo mawili either aanze Juma Abdul au Hassan Kessy hapa ni kocha kujitoa akili kwani katika mchezo wa Marudiano Kimataifa na Rollers Kessy hatacheza hivyo kocha anaweza  akaamua kumuanzisha kabisa Kessy ili Juma Abdul abaki salama kusubiri Wabotswana au kuamua kuanza  kabisa kumtumia Juma Abdul mapema ili kuingia mapema kwenye mipango  ya matumizi atakapokutana na Rollers

  Namba  3 ni wazi Gadiel bado amekuwa mzuri  zaidi hasa  kwenye ukabaji licha ya kutokuwa nzuri sana timu inaposhambulia kumlinganisha na Haji Mwinyi, Lakini kwa performance ya Haji Mwinyi mechi iliyopita naiona nafasi ya Gadiel katika mchezo wa Leo.

  Mabeki wa kati : Said Makapu na Kelvin Yondani ambao kwa Siku za karibuni wamekuwa wakicheza sana pamoja bado nawaona wakiendelea kuaminiwa katika mchezo wa Leo.

  Viungo wa kati : Naona Tshishimbi akirejea kikosini kucheza namba 6 au nane  itategemea kocha atamwanzisha kiungo gani mwingine kati ya Pato ambaye  alipotea mchezo uliopita, Kamusoko au Mama Edward ambaye aliingia sub mchezo uliopita na kuonekana kutulia kiasi kuliko Pato, kama ataanza Maka au Pato   Basi Tshishimbi atacheza namba 8, kama Ataanza Kamusoko ambaye anaonekana  bado hajawa fiti asilimia mia Basi Tshishimbi atacheza namba 6.

  Viungo wa pembeni : Namba saba kwa Siku za karibuni msomaji wa kwataunit.com amekuwa akicheza Emmanuel Martin ambaye amekuwa akitokea pembeni na kuingia na mipira eneo la kati ya uwanja naiona bado nafasi yake ya kuanzia kwenye Kikosi huku  namba 11 Ibrahim Ajibu ambaye alikuwa  na uwezo Mkubwa katika mchezo uliopita VPL dhidi ya Kagera nafasi yake haina Mashaka.

  Washambuliaji wa kati : Obrey Chirwa na Pius Buswita bado wanaendelea kuwa na nafasi ya kuanza katika Kikosi cha Yanga kitakachoshuka leo . kwa kikosi cha Leo endelea kutembelea site yetu tutaweka mapema sana kitakapotoka.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY