Kikosi cha Simba Kinachoweza kuanza dhidi ya Al Masry leo 17 March 2018

  0

  Kikosi cha Simba Kinachoweza kuanza dhidi ya Al Masry leo 17 March 2018

  Kulingana na wachezaji walioenda nchini Misri na mazoezi ambayo yamefanyika siku za mwisho mwisho kuelekea pambano kati ya Al Masry na Simba mtandao wa kwataunit.com tunakupa Kikosi cha Utabiri kinachoweza Kuanza leo.

  Golini : Aishi Manula bado ni kipa anayeaminiwa na ataendelea kuaminiwa kutokana na uwezo wake kuonekana bado kuwa mzuri lakini pia Uzoefu na mechi za kimataifa inaweza kuwa faida nyingine kulinganisha Said Mohammed Nduda.

  Mabeki wa pembeni: Kuna uwezekano mkubwa wa Kuendelea kuwatumia Nicolas Gyan na Asante kwasi kama beki wa Kulia na Beki wa Kushoto kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita.

  Mabeki wa Kati : Hakuna Shaka juu ya Nafasi ya mchezaji kiraka Erasto Nyoni kwenye eneo la beki wa Kati na bila shaka kwa Leo ataanza huku nafasi ya beki Mwingine wa Kati atacheza kati ya Mlipili au Juuko Murshid lakini kwa Leo nafasi ya Juuko Murshid ni kubwa zaidi kuanza na Erasto Nyoni.

  Viungo wa kati na pembeni: Hii ni nafasi nyingine kwa Wachezaji Jonas Mkude ambaye ni wazi kuwa ni fundi katika eneo la kati, Nafasi nyingine itakuwa kwa Shomari Kapombe ambaye alichezeshwa eneo la kati katika mchezo uliopita na hata mazoezi ya mwisho kabla ya timu kusafiri alionekana kucheza eneo hilo mazoezini.

  Wengine msomaji wa kwataunit.com ni Shiza Kichuya na James Kotei, Kotei akicheza kama namba 7 anaweza kusaidia eneo la katikati ya uwanja ambalo imekuwa kawaida kwa Simba kulitawala wakati Shiza Kichuya akitokea kama mchezaji Huru uwanjani kama ambavyo amekuwa akicheza siku za Karibuni  akiwa na Kikosi cha Masoud Djuma na kocha Mkuu Pierre Lechantre.

  Au kunaweza kukawa na Option ya kumwanzisha Kapombe kama namba 2 na eneo la kati kubadilika kwa kucheza Mkude, Kichuya, Kotei na Said Ndemla ambaye anaweza kusaidia kupiga pasi ndefu au kucheza mipira ya adhabu inayotokea uwanjani au hata kucheza mipira ya mashuti ya Kushtukiza ambayo Ndemla ni mzuri.

  Washambuliaji  : Katika eneo ambalo linatazamwa zaidi na washabiki wengi wa Simba ni eneo lao la Ushambuliaji kwani wanahitaji magoli zaidi ili kujihakikishia kupeta ni wazi Mganda Emmanuel Okwi ataanza kama Namba kumi akicheza na Nahodha John Raphael Bocco ambaye amekuwa mhimili mkubwa mbele.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY