Hivi ndivyo Simba ilivyokwepa Mitego mitatu ya Al Masry kabla ya Mechi

  0

  Hivi ndivyo Simba ilivyokwepa Mitego mitatu ya Al Masry kabla ya Mechi

  Klabu ya Simba jana ilicheza mchezo wake wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry huko Port Said nchini Misri mechi ambayo iliisha kwa sare ya Bila Kufungana na Simba kutupwa nje ya mashindano.

  Lakini kabla ya mchezo huo Simba walikwepa mitego karibu mitatu ambayo walihisi wanategwa na Al masry.

   

  Simba ilibidi watume watu mapema watafute Hoteli ambayo watafikia na kufanya mambo yao bila kufatiliwa na wapinzani wao timu ya AL Masry

  Chakula

  Licha ya kufikia katika hoteli lakini Simba msomaji wa kwataunit  hawakuwahi kula katika hoteli hiyo bali walikuwa wanalala na msosi walikuwa wanatafuta wanapojua wao ili kukwepa tu hujuma za Wapinzani wao Al Masry.

  >> Soma zaidi habari zetu hapa <

  Usafiri. 

  Kwenye Ishu ya Usafiri Simba walikuwa makini asikuambie Mtu kwani Toka wanafika Misri hawakutaka kutumia huduma ya usafiri kutoka kwa wenyeji wao, Ila utata zaidi ulikuja jana kabla ya Simba kwenda kwenye mechi.

  Simba walipelekewa Basi kwaajili ya kuwapeleka uwanjani lakini viongozi wakagoma Kulitumia wakihisi limepuliziwa madawa ambayo yangeweza kuwachosha wachezaji.

  Simba walilazimishwa kutumia basi hilo lakini Viongozi walikataa katakata wakisema watatumia usafiri wao binafsi wa kukodi, na hata baadaye viongozi wa Chama cha soka Misri nao walisimamisha basi la Simba saa moja kabla ya mechi lakini Simba walibaki na Msimamo wao wa kutotumia basi waliloletewa.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY