Yanga kusafiri kwenda Singida asubuhi Hii

  0

  Yanga kusafiri kwenda Singida asubuhi Hii

  Klabu ya Yanga ya Jijini Dar Es Salaam asubuhi hii imeondoka mjini Morogoro ilipokuwa imeweka Kambi ya Muda kujiandaa na mchezo kati yake na Singida United kuelekea mjini Singida.

  Yanga inaondoka kuwafata Singida United ambao nao wamekimbia Mji na kwenda kujificha nje kidogo ya Singida Huko Kiomboi wakijiandaa na mchezo dhidi ya Yanga.

  Yanga msomaji wa Kwataunit.com  inaondoka na wachezaji wake karibu wote kasoro Ramadhan Kabwili ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa Ya Vijana Ngorongoro Heroes  wanaojiandaa na Mchezo dhidi ya Congo kesho Jumamosi.

  Huku pia Yanga ikiendelea kuikosa Huduma ya Mshambuliaji wake Amis Tambwe ambaye bado hajawa fiti asilimia 100.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY