Haji Manara atoa ya moyoni kuhusu wachezaji waliosajiliwa Simba toka Azam

  0

  Haji Manara atoa ya moyoni kuhusu wachezaji waliosajiliwa Simba toka Azam

  Afisa Habari wa Timu ya Simba Haji Sunday Manara ameamua kutoa ya Moyoni kuhusiana na wachezaji wanne waliosajiliwa Simba kutokea Azam Fc.

  Simba wakati wa Dirisha Kubwa kabla ya Msimu wa Ligi Kuanza waliwasajili wachezaji wanne kutoka Azam Fc Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na John Raphael Bocco.

  Kupitia Ukurasa wa Instagram wa Haji Manara amepost video nahodha wa Simba John Boccoa akiahidi Ubingwa mbele ya wanachama wa Simba baada ya kutoka Misri huku Manara msomaji wa Kwataunit akiandika Caption Hii hapo chini

  ” Tulipowasajili hawa tulibezwa sana..ila nikiri.uwepo wa Aishi.Nyoni,kapombe na Boko umetuongezea kitu kwenye timu tena ndani na nje ya uwanja…wanajua kisha wanajitambua,..sahau kuhusu magoli ya Boko uwanjani,hebu msikilize le capetonho Boko akitoa ahadi kwa niaba ya wachezaji wenzie @manula_28 @john22raphael@kapombe_shomari @nyoni_erasto@vanmohamed @azamfcofficial”

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY