Habari mpya 3 kutoka Yanga usiku huu

  0

  Habari mpya 3 kutoka Yanga usiku huu

  Yanga wakitumia Ukurasa wake wa Twitter wametoa Habari Mpya 3 usiku huu ikiwa ni Mara baada ya kukusanya points 3 wakicheza dhidi ya Stand United kwa Ushindi wa bao 3 kwa 1 magoli ya Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajibu na Obrey Cholla Chirwa.

  Milango ya Kwenda Botswana

  Yanga wameandika kuwa timu Yao utaondoka kwenda Botswana usiku wa Leo kuwafata Township Rollers ambao ni wapinzani wao kimataifa safari ikiwa ni kwaajili ya mchezo wa marudiano baada ya ule wa awali Yanga kufungiwa bao 2 kwa 1 na Rollers.

  Katika taarifa hiyo jumla ya wachezaji 20 watasafiri kwenda Botswana.

  Yanga wawasogezea Huduma ya Habari zao wapenzi na washabiki wake

  Klabu ya Yanga usiku huu wametoa namna nzuri ambayo wapenzi , washabiki na wanachama wa Yanga watakuwa wakipata Habari kwa njia ya Simu kwa kujiunga kwa kutuma neno Yanga kwenda  15501 gharama ikiwa  shilingi 100 kwa Siku.

  Website ya timu itarejea baada ya matengenezo

  Yanga pia wametoa  taarifa usiku huu kuwa website itarejea hewani marekebisho yanayoendelea yakikamilika, Yanga msomaji wa kwataunit imekuwa  ikitumia Website hiyo kutoa taarifa zao.

   

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY