Bolasie wa Congo apagwa zaidi na Mchezaji Huyu Taifa Stars,Amtabiria Ulaya

  0

  Bolasie wa Congo apagwa zaidi na Mchezaji Huyu Taifa Stars,Amtabiria Ulaya

  Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Congo na Timu ya Everton Yannick Bolasie ambaye juzi kati alikuwepo Tanzania kwenye mchezo wa Kirafiki kati ya Tanzania na Congo mchezo ulioisha kwa Tanzania Kushinda bao 2 kwa 0 amemtaja nyota wa Stars na Kumtabiria Ulaya.

  Bolasie akizungumza baada ya Mchezo huo uliofanyika Jumanne March 27 katika uwanja wa Taifa amemtaja Kiungo wa Simba  Shiza Kichuya kuwa anauwezo mkubwa na Huenda akapata nafasi ya Kucheza nje ya Nchi (Ulaya)

  “Yule namba 16 nimeona anavitu vingi anapokuwa uwanjani vitu ambavyo vinaweza kumpa nafasi ya Kucheza ulaya, Akionekana kuna timu zinaweza kumchukua ” 

  Katika mchezo huo msomaji wa Kwataunit  Kichuya alishiriki katika Magoli yote mawili goli la kwanza akitoa Pasi ya Mwisho na Kisha Kufunga goli la Pili akipewa pasi na Mbwana Samatta.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY