Amka nayo Hii mpya kabisa kutoka Yanga kuelekea mchezo na Singida

  0

  Amka nayo Hii mpya kabisa kutoka Yanga kuelekea mchezo na Singida

  Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara Yanga ambao jana walisafiri kutoka Morogoro mpaka mjini Singida walifika salama.

  Baada ya Kufika Mjini Singida kwa siku ya jana Mwalimu George Lwandamina na Benchi lake la Ufundi lilishauri wachezaji wapumzike kwa Siku ya jana na watumie muda Huo kuzunguka maeneo mbalimbali ya Mji wa Singida ikiwa ni hali ya Kuzoea hali ya Hewa.

  Leo nini kitaendelea kwa Yanga?

  Baada ya Jana kutofanya mazoezi kabisa leo kikosi cha Mabingwa hao wa Ligi kuu mara 3 mfululizo kitafanya mazoezi katika uwanja wa Namfua kabla ya Kesho kumenyana na Singida United katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY